Friday, November 22, 2024

Top 5 This Week

Related Posts

“Slay Queens Who Slept With Your Husband Are Shading Crocodile Tears” Bodyguard Mourns Ababu’s Ex-Wife

Ababu Namwamba’s former bodyguard expressed anger at women pretending to mourn Priscah Mwaro yet they were caused her pain when she was alive.

Priscah Mwaro, the ex-wife of Sports CS Ababu Namwamba, died a few days ago.

Ababu’s former bodyguard who goes by the name Bondia Madaras on Facebook eulogized Priscah, revealing that she was depressed in her last days alive.

Habari za kifo chake Prisca Mwaro zimenifika kwa mshituko na mshangao mkubwa, nimeshikwa na butwa na bumbuwazi na kubaki na machungu sihaba mtimani. Kwa zaidi ya miaka 20 niliyomjuwa, tokea alipokuwa akichumbiana hadi kufika kuolewa na hata kuishi kama mke na mume kwa mdozi wangu wa zamani, sikuwai kumuita kwa jina, bali kila nilipo tumwa kwake ama yeye kunituma, nilimuita jina Madam.

Nilimpa heshima na tahadhima zinazo stahiki kipindi chote nilipokuwa mlinzi ( Bodyguard ) wa mumewe, tokea akiwa mchumba, mke hadi kutengana kwao, jina Madam lilisalia hivyo kuashiria heshima fufufu niliyo kuwa nayo kwake.

Katika shughuli za kampeni au hafla zote pariwanja, nje na ndani ya bunyala, niliakikisha anapata usalama dhabiti na wa kutosha katika hafla zote za kisiasa, harambee na hata burudani wakiwa na mumewe au pekeyake masaa yote, nilipohitajika. Prisca alikuwa nguzo na kiungo muhimu alie changia pakubwa kufanikisha safari ya siasa za mumewe kinyume na wanawake wengi humu nchini.

Kwa mda wa miaka yote niliyo kuwa karibu naye kwangu ilikuwa ni vigumu kujuwa kuwa Madam amekasiriaka, kwani kila wakati alikuwa mwingi wa kutabasamu hata mambo yalipokuwa magumu.

Licha ya kuwa wa umri wa barubaru, kwangu alikuwa mama na mzazi wangu tena asie na upendeleo. Kila ulipoenda kwake kwa nyumba kutembelea bwanake kwa shughuli za kikazi, jambo la kwanza atakuuliza kama umekula, na punde tu utakapo pepesa macho na kusitasita kujibu atakwambia kaa wakutengezee chakula ule kwanza, alikuwa mama mkarimu na wa moyo mzuri.

Na hata tulipo hitaji kitu kwa mumewe, angetushauri na kutupa siri ni wakati gani mzuri wa kumuomba bwanake kitu na tupate kwa haraka, hilo ni dhihirisho kuwa alipenda wafanyikazi wa bwanake na kuwachukuwa kama watoto wake.

Prisca kwa mara ya kwanza wacha nimuite kwa jina nikibubujikwa na machozi, alikuwa mwanamke shupavu japo aliishi na hofu na machungu mengi. Alikuwa mtu wa usiri tena hakupenda kusema na watu juu ya machungu yake. Bali kuna jambo lilimsibu na kumuongezea machungu zaidi kilichomfanya afunguke moyo na kunieleza yote.

Hivi karibu, alinitafuta messenger na kunieleza juu ya mambo yanayo mtatizo na kumpa uchungu zaidi moyoni, lakini alipoona sishikanishi, aliamua kunipigia simu akafungua moyo wake juu ya mambo yanayo mtatiza, tuliongea kwa takriban dakika 37 hivi, katika maongezi yake, kama mtu mzima nilihisi kuwa alikuwa na msongo wa mawazo ambapo alitaka ushauri nasaha kama tiba kwake, kama mfanyikazi wake wa kitambo, nilimtia moyo na kumpa motisha, kumpa tumaini na wasia. Kifo chake kimenishtua kwani sikujuwa kuwa mazungumzo hayo ndio ya mwisho.

Ninaomba serikali ifanye uchunguzi ili ibainike ni kipi kilicho pelekea kifo cha mwanadada huyu. Hakika inauma tena sana.
Sio mara moja tumeongea na mrembo huyu, hakika kifo chake kinaniuma.
Mungu ailaze roho yako mahali pema peponi mama.

In another post, Bondia Madaras confirmed that Ababu was cheating on Priscah with a bevy of slay queens as earlier reported by Kenya Reports. 

Bondia Madaras expressed anger saying that the same slay queens who wrecked Priscah’s marriage were busy shedding crocodile tears following her death.

“If the dead one can wake-up from the death today and read condolences from some people in social media, she can be shocked.

“Bondia Madaras I see many crocodile tears from some maslay queens, even those who were eating pizza, chips, drinking Johnson and slept with your husband with shameless eyes, they will mourn you and say how good you were when you were still a live.
“And they will dress very well at burial day, attending your burial and crying loudly with crocodile tears, wonders of the world shall never end, too much drama on social media. They better zip their mouth,” Bondia Madaras wrote.

 

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Popular Articles

Verified by MonsterInsights